Harmonize: Mke wangu arudi

HomeBurudani

Harmonize: Mke wangu arudi

Msanii na mmiliki wa lebo ya Konde Gang, Rajabu Abdul maarufu kama Harmonize amefunguka wazi na kueleza kwamba ameachana na mchumba wake Briana mrembo mwenye asili ya Australia na sasa anachotaka ni mke wake wa zamani (Kajala) arudi.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amesema amechana na Briana kutokana na kwamba kila mtu hataki kwenda kuishi nchi ya mwenzake na pia alimueleza msichana huyo kwamba bado anampenda Kajala.

Aidha, Harmonize amemtaka mtangazaji wa Clouds redio, Mwijaku kuacha kuingilia kwenye mahusiano yake huku akikiri kwamba ni takriban miezi mitatu sasa hawajazungumza kwahiyo hajui kitu chochote.

error: Content is protected !!