Ushauri wa Jahazi kwa Harmonize

HomeBurudani

Ushauri wa Jahazi kwa Harmonize

Watangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa kwenye redio ya Clouds, Mussa Hussein, George Bantu na Captain Gardner Habash wamempa ushauri msanii Harmonize kuhusu Kajala baada ya kuona jitihada anazotumia katika kurejesha penzi lao.

Wakizungumza kwenye kipindi cha Jahazi, watangazaji hao walisema anachotakiwa kufanya Harmonize ni kutuma hela kwa Kajala kwani wanaamini ana namba za akaunti ya benki za mrembo huyo kuliko kulalamika mitandaoni kama ambavyo anafanya.

“Tunajiuliza hana akaunti ya kajala? si akaunti yake anayo, dawa ni moja tu peleka mzigo, weka mzigo yani ni mzigo mpaka mwisho,” alisema Mussa Hussein.

Aidha, Juma Nature naye aliweza kuchangia kuhusu jambo hilo na kusema kuwa Kajala ni mkubwa kuliko Harmonize hivyo anachotakiwa kufanya ni kuangalia mtu wa kukaa naye na huenda bado hajamfahamu vizuri Kajala na ndio maana anashindwa kumpata na kurudisha penzi lao.

error: Content is protected !!