“Utafiti: Bodaboda inavyoweza kuharibu iPhone yako”

HomeElimu

“Utafiti: Bodaboda inavyoweza kuharibu iPhone yako”

Kama unataka Camera ya iPhone 12 yako iwe na ufanisi wa hali ya juu muda wote, basi unapaswa kuiweka mbali na “vibration” zitokanazo na pikipiki/bodaboda au mashine yeyote ile inayozalisha “vibration” kubwa kwani vitu hivyo vinaweza kupunguza ufanisi wa Camera yako.

Tahadhari hii imetolewa na chapisho kutoka kampuni ya Apple, linalosema kuwa teknolojia iliyotumika kutengeneza Camera hiyo ambayo inasaidia iPhone kupiga picha nzuri hata kama kitu unachokipiga picha kitakuwa katika mwendo (optical image stalization), inaweza kuathirika kwa “vibration”.

Apple wameendelea kusema kuwa, Vibration pia inaweza kuua uwezo wa camera yako wa kufanya “autofocus” yenyewe kwani teknolojia hiyo inatumia usumaku (magnetic sensors) kukingana na mvutano wa asili wa Dunia (Gravity) kuhakikisha kwamba chochote unachopiga picha kinatoka vizuri hata mkono wako unacheza.

Sasa basi, kuweka simu yako na vitu kama hivyo, kama kupanda pikipiki mara kwa mara na simu yako ikiwa mfukoni inaweza kupunguza ufanisi wa Camera ya iPhone 12 yako. Usafiri kama pikipiki huzalisha mtikisiko mkubwa (high vibrations) ambao Camera ya iPhone 12 ni ngumu kuhimili. Mtikisiko huo unaweza kusafiri kupitia mikono yako wakati unaendesha, au kupitia mwili wako moja kwa moja wakati umekalia pikipiki inayotembea na kufikia simu yako.

Apple wanashauri tutumie vifaa maalumu vya kupunguza mtikisiko (Vibration dampers) kadiri tuwezavyo tuwepo kwenyo vyombo kama pikipiki au tupunguze matumizi ya pikipiki mara kwa mara tukiwa na simu zetu kupunguza athari katika camera zetu.

 

error: Content is protected !!