Maajabu: Ujio wa Mbu vipofu, wasioona binadamu

HomeElimu

Maajabu: Ujio wa Mbu vipofu, wasioona binadamu

Kwa miaka mingi sasa binadamu amekuwa akiishi katika ugomvi mkubwa na Mbu. Kuishi na Mbu imekuwa ni tatizo kubwa sana kutokana na uwezo wa Mbu kuweza kubeba na kusambaza magonjwa mengi ambayo humdhuru binadamu kubwa ikiwa ni ugonjwa wa Malaria.

Zipo dawa ambazo huwaondoa Mbu kwa muda tu, lakini pindi tu dawa hizo zinaokoma kufanya kazi basi Mbu hurejea tena katika mazingira ya mwanadamu. Mpaka sasa hakuna njia sahihi za “kisayansi ambazo zimethibitika kuweza kumaliza kabisa tatizo la Mbu duniani.

Lakini utafiti uliochapishwa hivi karibuni na jarida la ‘Medical Journal Currrent Biology’ linatoa taswira mpya katika mapambano ya madhari yasababishwayo na Mbu.

Wanasayansi wanasadiki yakuwa upo uwezekano wa kuhariri vinasaba vya Mbu, na kuweza kuwafanya kuwa na upofu kuwafanya wasiweze kuwaona binadamu tu, na hivyo kupunguza uwezekano wa binadamu kuumwa na Mbu.

Wanasayansi hao wamesema kwa kutumia technolojia ya “Crisp-Case-Nine” wanaweza kumuondolea Mbu uwezo wa kumuona binadamu. Kumuondolea uwezo wa kumuona binadamu ni kumfanya akose chakula, hivyo kupoteza uwezo wa kuzaliana na hatimaye baada ya muda kupotea kwa muda kizazi hicho.

error: Content is protected !!