Rais Samia Hassan Suluhu leo Septemba 23, 2021 atahutubia mkutano wa 76 wa Baraza la Umoja jiijini New York, Marekani.
Historia inaonesha kuwa Tanzania imewahi kuwakilishwa mara 69 katika Baraza la Umoja wa Mataifa katika mikutano tofauti. Katika mara zote hizo hapakuwahi kutokea Tanzania kuwakilishwa na Mwanamke.
Kwa mara ya kwanza kabisa, Rais Samia anakwenda kuwa mwanamke wa kwanza kuzungumza katika baraza hilo kutoka Tanzania.
Hii ni rekodi ambayo inakwenda kuwekwa leo, na pia ni ishara ya kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia.