Vigogo Yanga watunishiana misuli, kila mmoja anataka kocha wake (Nabi, Zahera, Kaze)

HomeMichezo

Vigogo Yanga watunishiana misuli, kila mmoja anataka kocha wake (Nabi, Zahera, Kaze)

Timu ya soka ya Yanga ina makocha watatu  raia wa kigeni wenye sifa za kusimama kama makocha wakuu

Kocha Mkuu ni Mtunisia, Nasreddine Nabi lakini sasa aliyekuwa kocha wa timu hiyo kabla ya Nabi, raia wa Burundi Cedric Kaze amerejea nchini ikiaminika kwamba anajiunga na Yanga kama kocha msaidizi.

Pamoja na Nabi na Kaze, Yanga imemrejesha  Mwinyi Zahera ambaye aliwahi kuwa kocha mkuu wa ‘timu ya Wananchi’. Tetesi zinaeleza kwamba Zahera atasamiamia soka la vijana hapo Jangwani.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambacho hakikutaka kutajwa, Kaze amerudi kwa sababu baadhi ya viongozi wa timu hiyo wameanza kukosa imani na kocha Nabi, ndio maana ameletwa Kaze ambaye vigezo vyake vinatosha kabisa kuwa kocha mkuu. Iwapo Nabi atashindwa kufikia malengo ya timu hiyo, itakuwa rahisi kwa Kaze kukabidhiwa majukumu kama kocha mkuu.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba Cedric Kaze aliondoshwa Yanga akiwa hana rekodi mbaya sana, hivyo viongozi wa timu hiyo akiwemo ‘Engineer’ Hersi Said walipigia chapuo kurudishwa kwa Mrundi huyo.

Kwa upande wa Zahera, tetesi zinadai kwamba alirudishwa Yanga kwa ajili ya kuwa kocha mkuu kutokana na kuwa chaguo la baadhi ya wadhamini na viongozi wa timu hiyo, lakini lipo kundi la viongozi ambalo halilikubaliana na kumrejesha kama kocha mkuu.

Nabi anaendelea na kazi ya kuinoa Yanga, Mwinyi Zahera ameshaonekana akiwa na viongozi wa Yanga siku za hivi karibuni, Kaze ameshatua jijini Dar es Salaam.

Kinachosubiriwa ni uongozi wa Yanga kutoa taarifa rasmi kuhusu majukumu ya walimu hao.

 

error: Content is protected !!