Marais wa Tanzania waliowahi kutoa hotuba Baraza la Umoja wa Mataifa (UN)

HomeKitaifa

Marais wa Tanzania waliowahi kutoa hotuba Baraza la Umoja wa Mataifa (UN)

1. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (1961 – 1985)

Mwalimu Julius Nyerere ameshiriki mara tano katika Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa lakini amehutubia Baraza hilo mara mbili tu akiwa kama Rais, nazo ni;
– 27 Septemba 1985, Mkutano wa 40
– 30 Septemba 1983, Mkutano wa 38
Hizo mara tatu zilizobaki alipata tu fursa ya kujibu hoja ya kutoa mchango katika Mikutano husika.

2. Rais Ali Hassan Mwinyi (1985 – 1995)
– 8 Oktoba 1987, Mkutano wa 42
– 4 Oktoba 1994, Mkutano wa 49

3. Rais Benjamin William Mkapa (1995 – 2005)
Mkapa amewahi kudhuria Mikutano ya Baraza la Umoja wa Mataifa mara 13, kati ya hizo ni mara 3 pekee ndio aliweza kutoa hotuba kama Rais Mbele ya Baraza hilo. Mara 10 zilizobaki alichangia hoja, kutuma ujumbe au salamu kutoka Tanzania, akiwa kama Rais na Waziri wa Mambo ya Nje kwa nyakati tofauti.
– 21 Oktoba 2004, Mkutano wa 59
– 20 Septemba 1999, Mkutano wa 54
– 04 Oktoba 1996, Mkutano wa 51

4. Rais Jakaya Mrisho Kikwete (2005 – 2015)
Kikwete amehudhuria mara 13 Mikutano hiyo, na amehutubia mara mbili tu Baraza hilo, na zilizobaki amehudhuria pia kama Rais na Waziri wa Mambo ya Nje, lakini alitoa tu mchango, kujibu hoja katika vikao mbalimbali vya Baraza hilo.
– 29 Septemba 2015, Mkutano wa 70
– 22 Septemba 2011, Mkutano wa 66

Kwa Ujumla, Tanzania katika Mikutano ya Baraza la Umoja wa Mataifa imewakilishwa mara 69 na Marais, Mawaziri wa Mambo ya nje, Mabalozi pamoja na vingozi wengine waandamizi. Rais Samia Suluhu Hassan kwa mara ya 70 katika Mkutano wa 76, anaiwakilisha Tanzania kama muwakilishi Mkuu katika Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa jijini New York Nchini Marekani.

error: Content is protected !!