Sababu 5 za watu kutazama filamu za ngono

HomeElimu

Sababu 5 za watu kutazama filamu za ngono

Tabia ya kupenda kutazama filamu za ngono ni uraibu kama ulivyo uraibu mwingine. Yamkini wengi hawafahamu kama filamu hizi zina madhara kiafya hata katika mahusiano. Utafiti wa “Beata Bothe” unaonesha kwamba 5.94% ya watu wanaopenda kutazama filamu za ngono hutazama kutokana na kutoridhishwa kingono na wenza wao.

Lakini bado zipo sababu nyingine zinazoeleza kwanini watu wanapenda kutazama filamu za ngono.

  1. Kupandisha Ashiki
    Ifahamike kuwa, hili ndio lengo kuu la kutengeneza filamu za ngono. Wengi hutazama filamu za ngono kupandisha ashiki au hisia za kimapenzi kufikia matamanio yao. Kupata hisia za kimapenzi ni hitaji muhimu la mwili, lakini unapaswa kujua kuwa watengenezaji wa filamu hizi hawazingatii afya wala mahusiano ya mtazamaji pindi anatazama. Hivyo unapaswa kujua kwamba kutazama bila kuwa mwangalifu inaweza kukuletea madhara kiafya na katika mahusiano yako.
  1. Kujielimisha
    Kundi la watu ambao hutazama filamu za ngono ili kujifunza vitu kuhusu ngono. Utafiti wa “Bothe” unaonesha kuwa vijana 45% hutazama filamu za ngono kwa minajili ya kujifunza namna ya kufanya ngono. Pia chanzo hicho hicho kinaonesha kuwa watu wenye umri kati ya miaka 18 – 24 (24.5%) wamesema kuwa filamu za ngono ni nzuri sana kwa kujifunzia ngono.
  1. Kukingana na hisia mbaya
    Mtu anapokuwa na msongo wa mawazo, mkazo au sonono, utafiti unaonesha kuwa ni rahisi sana mtu huyu kujikuta ameingia kwenye tabia ya kutazama filamu za ngono. Utafiti unaonesha kuwa filamu za ngono hazina msaada huo kama wengi wanavyodhani, bali filamu hizo baada ya muda zinaongeza mawazo badala ya kupunguza.

    > Njia 6 za Uhakika za kuacha Punyeto/Nyeto/Puchu

  1. Kuondoa uchovu
    Utafiti unaonesha kwamba wanawake wengi hata wanaume hupenda kutazama filamu za ngono wanapokuwa wamechoka. Filamu hizi kuzalisha homoni ambazo humpa mtazamaji uchangamfu wa muda tu. Lakini kimsingi ni kwamba filamu hizi baada ya muda zitakuwa zinachosa zaidi kuliko kuchangamka.
  1. Ni ngumu kuacha
    Kwa mujibu wa tafiti ni ngumu sana kuacha kutazama filamu za ngono kutokana na “raha” azipatazao mtazamaji. Huu ni  uraibu kama ulivyo uraibu wa vitu vingine, ni ngumu sana mtu kuacha kutokana suala hilo hutegemea namna ambavyo akili au ubongo wa mtu umeathirika kwa kiasi gani na filamu hizo. Kuacha inaweza kuwa ngumu sana, na inaweza kumgharimu mtu hata miaka mingi hata kama ataingia katika ndoa, bado tatizo hili linaweza kumuandama.
error: Content is protected !!