Mwanafunzi afariki baada ya kujirusha ghorofani

HomeKitaifa

Mwanafunzi afariki baada ya kujirusha ghorofani

Manawa Horera mwanafunzi wa mwaka wa pili wa kitivo cha Shahada ya Uhasibu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amefariki baada ya kuanguka kutoka kwenye ghorofa ya hosteli za chuo hicho katika harakati za kukimbia baada ya kudaiwa kuiba kompyuta mpakato (Laptop).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, ilisema kijan ahuyo akiwa kwenye harakati za kukimbia baada ya kuiba laptop aliruka kutoka ghorofa ya pili hosteli za chuo hicho maarufu kama Hosteli za Magufuli na kuumia.

“Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 8:00 usiku maeneo ya Hosteli za Magufuli Ubungo Dar es Salaam, ambapo kijana huyo wa miaka 22 aliingia kwenye chumba cha mwanafunzi mwenzake, Hamza Abdulrahman na kuiba kompyuta mpakato aina ya HP.”

“Alipobaini ameonekana na wanafunzi wenzake aliamua kuruka kupitia dirishani kutoka ghorofa ya pili kilipo chumba hicho na kudondoka chini, hivyo kuumia vibaya maeneo mbalimbali ya mwili wake lakini alikufa akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili.” alisema Muliro.

Aidha, Kamanda Muliro amewataka wanafunzi kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwa maeneo hayo ya hosteli yamekuwa na malalamiko mengi ya wizi.

error: Content is protected !!