Leo katika historia: Mali za Osama bin Laden zinataifishwa

HomeElimu

Leo katika historia: Mali za Osama bin Laden zinataifishwa

Mwaka 1954 uwanja wa mpira wa miguu wa Camp Nou unaochukua mashabiki 99,000 ulifunguliwa jijini Barcelona huko Hispania. Ndio uwanja mkubwa zaidi Ulaya na wa 11 duniani.

Tarehe kama ya leo mwaka 1974, Guinea Bissau ilitangaza uhuru wake kutoka kwa Ureno. Guinea Bissau ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Guinea Ureno, ilikuwa miongoni mwa vituo vya biashara ya utumwa ya wazungu katika karne ya 17 na 18. Guinea Bissau iko Kaskazini Magharibi mwa Afrika na katika pwani ya Bahari ya Atlantic.

Mwaka 2001 Rais George W. Bush wa Marekani aliagiza kutaifishwa kwa mali za watu na taasisi 27 waliotuhumiwa kujihusisha na ugaidi, akiwamo kiongozi wa al Qaeda, Osama bin Laden.

error: Content is protected !!