Sote tunajua kuwa muda ni kitu muhimu sana katika kazi au majukumu ya kila siku na kila kitu katika dunia hii kinakwenda na kutengemea muda. Muda ni zawadi ya dhamani tuliyopewa na Mwenyezi Mungu, lakini wengi wetu tumekuwa tukichezea zawadi hii.
Tunachezea muda sababu ya uvivu, hatuna malengo sahihi, hatuna ratiba sahihi yakukamilisha mambo yetu na pia kuwa au kufanya vitu visivyo na msingi. Uwezo wa mtu kufanya kitu na kukamilisha ndani ya muda kunasaidia kufikia malengo yake kwa muda sahihi kwa haraka.
Kwa mtu anayepata shida kwenda na muda na kufanikisha malengo basi leo tumekuletea njia tatu zitakazokusaidia kuwa ndani ya muda na kukamilisha mambo yako vizuri.
TENGA MAJUKUMU YAKO YA MUHIMU
Kuna msemo unasema “yeye ashindwaye kupanga muda, basi amepanga kufeli.” Mtu unapojua kupanga muda basi utafanikiwa kwa kile kitu ulichopanga. Ni vizuri ukapanga majukumu yako muhimu na muda hii itakusaidia kukamilisha mambo yako.
Ukiwa mtu wakupanga muda itakupa urahisi kukamilisha yale yote uliyoyatenga. Lakini usiwe tu mtu wakutenga muda na majukumu pia uwe unafuatilia na kuangalia kuwa wakati huu ni wakufanya jambo hili au lile.
WEKA MAWAZO (STRESS) PEMBENI
Hakuna jambo ambalo utaweza kufanikiwa bila kupata mawazo. Katika kila mafanikio lazima upate msongo wa mawazo, mfano mfanyabiashara akiwa anataka kuuza bidhaa zake atawaza wapi apeleke, na katika mzunguko huo lazima atapata matatizo ya hapa na pale yatakayomfanya awe na mawazo hata kuanza kukata tamaa. Ikumbukwe katika mafanikio ni MWIKO kukata tamaa, hivyo basi unachotakiwa kufanya ni kusonga mbele na kuendeleza kile ulichokianzisha.
NJIA NZURI ZA MAWASILIANO
Unapokuwa na njia nzuri za mawasiliano inasaidia kukufikisha katika malengo uliyoyaweka. Unapokuwa na ofisi wewe kama bosi inabidi uwe na mawasiliano mazuri na wafanyakazi wako ili kuleta umoja na mshikamano.
Itakusaidia kufikisha malengo yenu pale mlipotajaria, lakini ndani yenu kukiwa hakuna mawasiliano mazuri basi hapo mtapoteza muda badala ya kufanya kazi. Hivyo basi ni vyema ukahakikisha ndani yenu kuna mawasiliano mazuri.
Hizo ni baadhi ya njia zitakazokusaidia katika kuhakikisha unajua kutenga muda na kufikia malengo yako.