Biashara ya ngono imebadilika kutokana na changamoto mbalimbali kama UVIKO-19 pamoja na maendeleo ya teknolojia ambapo wadada wanafanya biashara hiyo kwa kutumia simu kupata wateja pamoja na kutoa huduma.
Mwanasafari kutoka Kenya ni miongoni mwa wasichana waliopata changamoto ya udhalishaji wa mtandao baada ya moja kati ya mteja wake kuvujisha video ikimuonesha mwanasafari akiwa anatoa huduma ya ngono.
Mwanasafari anasema “Mimi ni mama wa watoto wawili na nina mume wangu ila kutokana na changamoto za UVIKO 19 niliamua kusaidia uchumi wa familia yangu kwa kufanya biashara ya ngono kupitia simu tena kwa siri sana.
Ni miezi nane imepita tragu video ivuje sijui video imesambazwa kwa watu wangapi na makundi mangapi ila familia yangu haitaki kuniona na mume wangu amenikimbia.” ameeleza mwanamama huyo ambaye jina lake limebadilishwa ili kumhifadhi.
Amesema kila simu yake inapotoa mlio wa ujumbe mpya kufika, huwa anaogopa kufungua kwa sababu anajua itakuwa mtu mwingine anamtumia video hiyo iliyosambaa sana mitandaoni.