Hili hapa agizo la Serikali kwa wafanyakazi wa kigeni SGR

HomeKitaifa

Hili hapa agizo la Serikali kwa wafanyakazi wa kigeni SGR

Serikali kupitia, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, ameliagiza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kupitia upya vibali vya wafanyakazi katika ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) kutokana na kuwapo kwa wafanyakazi 732 wa kigeni wasio na vibali vya kazi na kusababishia serikali hasara.

Katambi alisema kwa sasa wafanyakazi hao wanalipa kodi ya Dola 200 za Kimarekani (shilingi 461,000) kwa na kutokuwa na vibali ambapo walitakiwa kulipa dola 1,000 (shilingi 2,305,000) na kupelekea serikali kupata hasara ya takribani dola 800 (shilingi 1,844,000) kwa kila mfanyakazi.

“Katika kila mmoja kati ya wafanyakazi 732 tumepata hasara ya dola 800 za kimarekani. Sasa naagiza kwamba ufanyike utaratibu kukagua upya vibali vya wafanyakazi wote ili tuweze kupata fedha ambazo zitasaidia wananchi katika miradi ya maendeleo,” ameagiza.

error: Content is protected !!