Fahamu siri 10 za kuboresha kumbukumbu yako

HomeElimu

Fahamu siri 10 za kuboresha kumbukumbu yako

  1. Jifunze kufanya kazi moja kwa wakati
    Kwenye mchakato wa kujifunza mambo mbalimbali hakikisha unajifunza jambo moja hadi ulimalize ndio uanze lingine. Kufanya mambo mengi kwa muda mmoja ni maandalizi ya kukufanya kuwa msahaulifu mzuri tu baadae pindi utakapojaribu kukumbuka ulipojifunza.
  2. Tafuna Bazoka (chewing gum)
    Wakati unafanya kazi au jambo fulani basi hakikisha unatafuna bazoka ili kuimarisha kumbukumbu zako. Kwa mujibu wa masuala ya saikolojia wanasema kuwa utafunaji wa baroka hufanya misuli ya ubongo kuchangamka hivyo kuboresha uwezo wa kukumbuka.
  3. Fanya mazoezi ya viungo
    Mazoezi mepesi kama kukimbia, kuruka kamba, kuogelea na kuendesha baiskeli ni aina ya mazoezi ambayo ni bora sana katika kuimarisha uwezo wa kukumbuka mambo. Mwili unapochangamka vizuri, huboresha afya akili na kumfanya mtu awe sawa kiakili hivyo kuboresha uwezo wa kukumbuka mambo.
  4. Kunja ngumi
    Pindi unapojifunza kitu kipya au unapojaribu kukumbuka kitu fulani, jaribu kukunja ngumi kwenye moja ya mkono wako. Hii inaweza kukustaajabisha kidogo, lakini utafiti unaonesha kuwa kwa watu wanaokunja ngumi wakati wa kujifunza jambo au kukumbuka jambo fulani, huwa na uwezo mzuri sana wa kukumbuka kuliko wale ambao hawakunji ngumi.
  5. Punguza Ulevi
    Unywaji wa pombe huathiri chembe hai (cell) za ubongo kwa kiasi kikubwa sana. Uharibifu huu hupelekea tatizo la usahaulifu au kupoteza kumbukumbu baada ya muda fulani. Washauri wa masuala ya saikolojia wanashauri kuwa kama mtu anataka kilevi kidogo, basi atumie mvinyo utokoanao na matunda kama zabibu na kadhalika kwa kiasi kidogo.
  6. Lala muda wa kutosha
    Binadamu anatakiwa kulala angalau kwa saa 7 hadi 9 kwa siku. Kulala muda mwingi huupa ubongo muda wa kutosha wa kupumzika baada ya mihangaiko ya muda mrefu. Kutopata usingizi wa kutosha ni moja ya sababu ambayo inapelekea mtu kuwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu.
  7. Michezo ya kutumia akili
    Ipo michezo ambayo hutumia sana akili kuicheza, michezo kama ‘Playstation’, draft, chess, bao la kete, keram na kadhalika. Michezo huchangamsha akili hivyo kuboresha uwezo wa kufikiria.
  8. Epuka msongo wa mawazo
    Msongo wa mawazo, sonona au mkazo (Stress) ni moja ya matatizo ya kiakili ambayo yanaweza kusababisha uwezo wa mtu wa kukumbuka mambo kupungua kwa kiasi kikubwa sana. Mtu anapokuwa na msongo wa mawazo chembe hai zake kwenye ubongo huathirika sana, hivyo baada ya muda tatizo hilo huathiri kumbukumbu zake.
  9. Lishe Bora
    Vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kama vile samaki, matunda na mbogamboga ni muhimu sana kwa ustawi wa mwanadamu. Hata hivyo virutubisho hivi ni muhimu sana kwa kuboresha kumbukumbu za mtu. Hivyo inashauri virutubisho hivi vitumike kwa wingi wa mtu anayetaka kuboresha uwezo wake wa kufikiria na wale walioathirika tayari na tatizo la kupoteza kumbukumbu.
  10. Acha kupiga punyeto
    Punyeto hupelekea ubongo kuwa na upungufu wa homoni inayoitwa ‘acetrycholine’, homoni hii kazi yake kubwa ni kufarisha taarifa kwenye chembe hai za mwili wa mwanadamu. Homoni hii ikipungua zaidi, husababisha upotevu wa kumbukumbu pamoja na kukosa umakini kwenye kufanya kwenye kutekeleza majukumu mbalimbali.
error: Content is protected !!