Waiba jeneza msikitini

HomeKitaifa

Waiba jeneza msikitini

Watu wasiojulikana katika kijiji cha Rivango, kata ya Mchauru, wilayani Masasi mkoani Mtwara, wamevunja mlango wa msikiti na kuiba jeneza linalotumika kwa ajili ya shughuli za maziko na kutoweka nalo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Rivango, Shabai Mohamedi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba tukio hilo limetokea usiku wa Machi 5 wakati waumini wakiwa tayari wameshaondoka baada ya kuswali ibada ya saa mbili usiku.

Akilaani kitendo hiko alisema waumini wa kiislamu wa kata hiyo na maeneo mengine ya jirani wanatarajia kukutana na kufanya dua ya pamoja kuwataka wahusika wa tukio warejeshe jeneza hilo mara moja.

“Tutafanya dua ya pamoja viongozi wa dini kuhusu jambo hilo ili matukio haya na mengine maovu ndai ya kata yetu yasiwe yanafanyika tena maana yamezidi kushamiri sana,”

“Tunaoomba ushirikiano kutoka kwa wananchi tuunganishe nguvu zetu kuwasaka waliohusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,” alisema Mwenyekiti Mohamedi.

 

error: Content is protected !!