Mwanafunzi wa chuo Kikuu auawa na aliyekuwa mpenzi wake

HomeKimataifa

Mwanafunzi wa chuo Kikuu auawa na aliyekuwa mpenzi wake

Mvulana mmoja nchini Kenya amemchoma kisu hadi kumuua aliyekuwa mpenzi wake aliyejulikana kwa jina la Mercy ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Laikipia.

Mashuhuda wanaeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa akifika mara kwa mara maeneo ambayo mpenzi wake alikuwa akiishi hadi pale walipotengana rasmi. Majirani wanaeleza kuwa  kulikuwapo na kelele ambazo ziliashiria vurugu au majibizano makali kila pindi mvulana huyo alipofika sehemu alipokuwa anaishi na mpenzi wake. Hata majirani walipoingilia kati kutaka kujua kulikoni, waliwaeleza kuwa hakuna tatizo kubwa na walieleza kuwa walikuwa wanaweka tofauti zao sawa.

Siku ya Jumatano mvulana huyo alifika tena katika makazi ya mpenzi wake na kujifungia ndani mwake, kisha kumchoma kisu mara kadhaa hadi msichana huyo kupoteza maisha. Majirani walifika hapo kutoa msaada baada ya kusikia kelele, lakini hata baada ya kufika eneo hilo walikuta mlango umefungwa kwani mvulana aliyetekeleza mauaji hayo akiwa bado ndani ya nyumba.

Muuaji alijaribu kujitoa uhai wake kwa kujichoma visu mara kadhaa maeneo ya shingoni na tumboni lakini watu walivunja mlango na kuwakuta wote wawili wakiwa chini na damu nyingi ikiwa imesambaa kwenye sakafu. Jeshi la Polisi lilifika kwa wakati na kufanikiwa kumuwahisha mvulana kituo cha afya ambapo iliripotiwa baadae kuwa anaendelea vizuri na polisi wataanza kuchukua maelezo yake.

error: Content is protected !!