Maneno 150 yaongezwa kwenye misamiati ya kiswahili

HomeKitaifa

Maneno 150 yaongezwa kwenye misamiati ya kiswahili

Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) limefanikiwa kuongeza misamiati mipya 150 kwenye Toleo la tatu la Kamusi Kuu ya Kiswahili kama hatua ya kukikuza Kiswahili.

Mabadiliko ya haraka ya matumizi ya Kiswahili na masuala ya sayansi na teknolojia yamechochea mabadiliko hayo, yameelezwa leo na Kaimu Katibu Mtendaji wa BAKITA Consolata Mushi wakati wa Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani.

Misamiati iliyoongezwa imetokana na maneno ya kiutamaduni, sayansi na teknolojia, siasa na maneno yanayotokana na UVIKO-19.

Kati ya maneno 150 yapo yafuatayo;

UVIKO– Ugonjwa wa Virusi vya Korona

Kigosigosi– Sehemu ya nyuma ya shingo ya kiumbe

Shitariki

1. Mfumo wa kujisajili na kulipia huduma kwa kipindi maalum ama mwezi, wiki au zaidi.
2. Jisajili na lipia huduma kama vile simu au magazeti katika kipindi maalum

Kibwiko– kishimo katika tonge la ugali

Demka

1. Cheza ngoma au dansi za mtindo wa kuzungusha shingo
2. Kucheza dansi au ngoma kwa ustadi mkubwa.

Idhaa zilizoshiriki ni pamoja na Radio Sauti ya Injili Congo, Redio China Kimataifa, Redio TV Buntu na BBC Swahili

error: Content is protected !!