Diamond: Mwijaku ananitumia message

HomeBurudani

Diamond: Mwijaku ananitumia message

Msanii na mmiliki wa lebo ya Wasafi, Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni ameachia EP yake ya First Of All (FOA) ameweka wazi kwamba hana chuki wala ugomvi na mtu yoyote na pia hushangaa kwanini baadhi ya watu wanakua wakimsema ilhali yuko nao sawa.

Amesema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye redio ya Wasafi na kuulizwa kuhusu baadhi ya watu kama Mwijaku, Carrymastory na Mange Kimambi namna wanavyokuwa wakimuongelea kwenye mitandao ya kijamii.

“Sio kila mtu akinizungumzia mimi vibaya labda ana ubaya na mimi, mwingine maskini ya Mungu anasema tu labda ndio njia yake yakutafutia ridhiki , kuna watu wengine njia zao ili wapate ridhiki lazima waniseme mimi na mimi nawasamehe nao fresh tu. Nitakupa mfano, mtu kama Mwijaku mimi Mwijaku ananitumiaga message labda kiongozi vipi shwari…namwambia kwenye Wasafi Bet promotion unaendesha vizuri unaua sana , i don’t take it personal,” alisema Diamond.

Aidha, Diamond ameweka wazi kwamba yeye hana shida na mtu yoyote yule anayeamua kumsema sehemu yoyote ile.

error: Content is protected !!