Show ya Kizz Daniel Tanzania yaingia doa

HomeBurudani

Show ya Kizz Daniel Tanzania yaingia doa

Usiku wa kuamkia leo August 8,2022 Jiji Dar es Salaam kumefanyika show ya SummerApplified ambapo msanii wa muziki kutokea nchini Nigeria Kizz daniel alitegemewa kutumbuiza kwenye show hiyo lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo

Pamoja na Kizz Daniel kutua kwenye ardhi ya Tanzania staa huyo hakufanikiwa kufanya show hiyo. Sababu za Kizz Daniel kutotokea Jukwaani hazijafahamika mpaka sasa. 

Pamoja na Kizz Daniel kutotokea jukwaani mastaa wengine kutokea nchini Tanzania kama Marioo, Saraphina, Mabantu na Young lunya walifanikiwa kutoa burudani kwenye show hiyo.

Kiingilio cha Show hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa WareHouse zamani Nextdoor kawaida ilikuwa ni shilingi 80,000 na VIP ni shilingi150,000.

error: Content is protected !!