Leo katika historia: Japan yazindua treni ya mwendokasi 1964

HomeElimu

Leo katika historia: Japan yazindua treni ya mwendokasi 1964

Tarehe kama ya leo mwaka 1960, nchi ya Nigeria ilipata uhuru wake. Wareno waliwasili Nigeria karne ya 15 wakifuatiwa na mkoloni Mwingereza aliyewasili katika nchi hiyo karne ya 16. Ilipofika karne ya 17 ardhi ya Nigeria iligeuzwa na kuwa moja kati ya vituo muhimu vya biashara ya utumwa hali iliyodumu hadi mwishoni mwa karne ya 19 ambapo vikosi vya majeshi ya Uingereza, viliidhibiti kikamilifu ardhi ya Nigeria. Hatimaye baada ya kupitia misukosuko mingi, Nigeria ikajipatia uhuru tarehe kama ya leo.

Mwaka 1964: Treni ya mwendokasi ilizinduliwa nchini Japan kwenye maandalizi ya Mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Tokyo. Treni hiyo ilienda kilomita 210 kwa saa.

Mwaka 1847 Mvumbuzi wa Kijerumani, Werner von Siemens alianzisha kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Siemens iliyotoa mchango mkubwa kwenye ugunduzi wa simu za mkononi.

error: Content is protected !!