Wanakijiji wapiga mawe gari la Mkuu wa Wilaya

HomeKitaifa

Wanakijiji wapiga mawe gari la Mkuu wa Wilaya

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ameagiza kukamatwa baadhi ya wanakijiji cha Engaroji kuwa kupiga mawe gari ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli.

Wanakijiji cha Engaroji walifanya kitendo hicho baada ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe kumkaripia Mwenyekiti wa Kijiji chao, Ngalama Mapena. Mwaisumbe alimkaripia kwa ghadhabu Ngalama kwa kushindwa kuwasilisha ripoti au taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji cha hicho kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

> Leo katika historia: Japan yazindua treni ya mwendokasi 1964

Kitendo hicho kiliwakarahisha wanakijiji kisha walichukua uamuzi wa kuanza kupiga kwa mawe gari lake.  Kiongozi huyo aliondoka kwa haraka katika eneo hilo kuepusha madhara zaidi kwa gari yake na yeye mwenyewe. Ripoti zineleza kwamba Mwaisube hakupata majeraha yoyote kutokana na tukio hilo.

Licha ya kutupia mawe gari ya Mkuu wa Wilaya, wanakijiji pia waliripotiwa kuvamia makazi ya watu na kuharibu mali zao. Tukio hilo limelaaniwa vikali na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na ameagiza hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa watu wote waliohusika kwenye udhalimu huo.

error: Content is protected !!