Ijue nyota yako leo Oktoba 08, 2021

HomeNyota

Ijue nyota yako leo Oktoba 08, 2021

NDOO (Jan 21 – Febr 19): Ifanye siku ya leo kuwa ni muhimu kwako pamoja na waliokuzunguka. Andaa mipango ya kuwa karibu na wapenzi wako. Kutoa zawadi ni muhimu kwako kwa kusaidia wengine. Jaribu kukutana na rafiki zako ukiwa na nafasi.

SAMAKI (Feb 20 – Machi 20): Mwaka unaendelea kupungua, tegemea mabadiliko makubwa kwa upande wako. Utaonekana na msongo wa mawazo ambao unahitaji mapumziko. Kukutana na wengine na kubadilishana mawazo ni jambo muhimu kwako.

KONDOO (Machi 21 – April 20): Achana na ukimya ambao unaweza kukuingiza katika mazonge na mitego ya kiusalama. Ni wakati wa kjitathmini na kupanga mipango yako kwa umakini. Wape mawazo yako wengine, yana tija sana.

NG’OMBE (April 21 – Mei 21): Kipaji chako ni chenye mafanikio. Uko tayari kufanya kazi kwa bidii na mafanikio. Usikubali kurejeshwa nyuma kutokana na mawazo kutoka kwa wengine. Una uwezo wa kugeuza mawazo yao kwa mafanikio.

MAPACHA (Mei 22 – Juni 21): Una uwezo wa kubadilisha hali iliyopo na kuwa na mafanikio kwa upande wako. Chukua muda wa kumsikiliza mpenzi wako. Usitumie muda zaidi kwa mapenzi kuliko kupanga mipango ya maendeleo. Kuwa makini sana.

KAA (Juni 22 – Julai 22): Maisha yaonekana kwenda vyema, japo yaonekana matatizo ya familia yanaweza kupunguza kasi ya mafanikio kwako. Wasiwasi wako pia waweza kukutia hofu ya maendeleo. Zungumza na watu wako wa karibu kwa kubadilishana mawazo na kuangalia mwelekeo.

SIMBA (Julai 23 – Aug 23): Jiepushe na mambo mengi yanayohusu fedha na matumizi. Ni kipindi cha kupunguza madeni mengi yaliyokukabili ili uweze kuendana na hali ijayo. Ukihitaji kununua kitu kwa sasa yapaswa ujiulize, jee kitu hiki kina umuhimu wowote kwangu?

MASHUKE (Aug 24 – Sept 23): Angalia katika jambo lisilo la kawaida kwako. Utavutia wengi kwa utekelezaji wa mambo yako. Kutambulika kwako ni jambo muhimu sana. Usiruhusu kuzongwa na matatizo ya kifamilia pamoja na wasiwasi.

MIZANI (Sept 24-Okt 23): Athari waliyonayo wengine juu yako ni kubwa sana, jenga tabia ya kujiepusha na shaka kutoka kwa wengine. Kuwa makini tabia za wengine ni ngumu kufahamika. Upande mwengine wa maisha uko vyema hasa katika suala la upendo.

NGE (Okt. 24 – Nov. 22): Kipindi cha misukosuko kinaonekana kupungua kwa upande wako. Bado sio kipindi chema kwako licha ya wingi wa jitihada unazojaribu kuonyesha. Acha mipango yako muhimu hadi kesho. Kuwa mwangalifu.

MSHALE (Nov. 23 – Dis. 21): Utulivu ni jambo muhimu kwako, tumia muda mwingi kufikiria mabadiliko katika upeo mkubwa. Wote wanaokujali, akiwemo mpenzi wako, wako tayari kukupa msaada mkubwa. Lengo ni kufanikisha amani na utulivu kwako.

MBUZI (Dis 22 – Jan 20): Madai kutoka kwa watu wako wa karibu pamoja na shughuli za nyumbani utazipata uzito wa kutosha. Matarajio ya mwisho wa wiki ni kipindi cha furaha na capricom chenye mategemeo. Umefanya mambo mengi katika kipindi kifupi na yenye kuthaminiwa.

error: Content is protected !!