Lulu na Wema Sepetu, Paka na Panya

HomeBurudani

Lulu na Wema Sepetu, Paka na Panya

Mwigizaji filamu maarufu nchini Tanzania, Elizabeth Michael (Lulu) ameweka wazi kuwepo kwa tofauti kati yake na mwigizaji mwenzake Wema Sepetu baada ya kuulizwa nini kinaendelea kati ya wawili hao.

Tofauti kati yao inasemekana kuanza baada ya Wema kupitia kipindi chake cha Cook with Wema Sepetu kumuuliza Mama yake Kanumba swali la nani kamuua mwanae na Mama huyo bila kukwepesha akamtaja Lulu.

“Aliwahi kunitumia meseji sikuwahi kuzijibu na kuanzia hapo hatujawahi kuwasiliana, yeye haoni kama amekosea nadhani pengine hapo ndo ubinadamu wangu uliponishika.” alisema lulu.

Lulu amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa duka lake jipya la mavazi la LizyPayLess lililopo Sinza Kwa Remi.

error: Content is protected !!