Milioni 10 kwa atakayempata Rubani aliyepotea

HomeKitaifa

Milioni 10 kwa atakayempata Rubani aliyepotea

Shirika la Ndege la PAMS, limetangaza donge nono la shilingi milioni 10 kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa rubani Samwel Gibuyi wa ndege 5H- WXO iliyopotea Oktoba 18, mwaka huu katika kituo cha Kiuma wilayani Tunduru majira ya saa 09:09 alasiri akiwa katika Hifadhi ya Pori la Akiba Selous Kingupira wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Meneja Mradi wa Shirika hilo ukanda wa Kusini, Oscer Bubambezi alibainisha kuwa kwa bahati mbaya Rubani Gibuyi hakufika katika kituo alichokuwa amekusudia kwenda huku akisisitiza kuwa hali hiyo imewatia wasiwasi na kuwafanya waripoti katika mamlaka ya anga Tanzania ili wasaidiwe kufanya doria za ardhini na angani kumtafuta katika pori hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru , Julius Mtatiro, alithibithisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba juhudi za kuitafuta ndege hiyo pamoja na rubani wake zinaendelea kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia ndege tano zinazopati angani, magari, pikipiki na watu wanaotembea kwa miguu katika pori hilo.

error: Content is protected !!