Eluleki Haule kutoka shule ya St Anne Marie Academy aliyeibuka kama mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la Saba amesema ndoto yake ni kuwa mpelelezi na kufanya kazi kwenye Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).
“Awali nilikua natamani sana kufanya kazi ya urubani na ilikuwa shauku yangu ya muda mrefu lakini hivi karibuni nimeona nibadili sasa natamani kuwa mpelelezi tu.” alisema Eluleki.
Akiongelea kuhusu siri ya mafanikio yake Eluleki alisema ni kuwa makini darasani, kufanya mapitio ya masomo mara kwa mara, nidhamu na kujituma kwenye masomo pamoja na kumcha Mungu wakati wote.
Mama mzazi wa Eluleki, Digna Mlengule amesema kwa sasa mtoto huyo anasoma masomo ya kuingia kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya Wavulana Marian ya Bagamoyo mkoa wa Pwani ila atajadiliana na baba yake ili waone kama aendelee kwenye shule hiyo au wampeleke shule nyingine.