Jumapili ni moja ya siku ndani ya wiki, iko baina ya Jumamosi na Jumatatu. Siku ya Jumapili kiutamaduni wa sehemu kubwa duniani, ni siku ya mapumziko, ambapo shughuli nyingi za uzalishaji husimama kwa siku hiyo, na watu kutumia muda huo kwa ibada, mapumziko, starehe au kutoka na familia kuvinjari maeneo mbalimbali.
J’pili hutambulika na kama siku ya kwanza ya wiki. Miongoni mwa waumini ya Dini ya kikiristo, siku hii ni kubwa kwao, ni siku ya Mungu kwa mujibu wao ni siku ya Mungu na siku ya ufufuo wa Kristo. Kanada, Uingereza, Uchina, Japani na Uphilipino na hata Amerika Kusini, J’pili ni siku ya kwanza ya wiki.
Shirika la Viwango Duniani (ISO) lenye makao yake makuu nchini Uswizi, linaichukulia J’pili kama siku ya mwisho ya wiki.
Ilikuwaje sasa Jumapili ikawa siku ya mapumziko?
Utamaduni maarufu duniani wa kuifanya siku ya Jumapili kuwa ni siku ya mapumziko ni utamaduni wa kirumi. Mwaka 321 Machi 7 Mfalme Constantine wa kwanza ambaye ndiye Mfalme wa kwanza aliyeukubali Ukristo Roma, alitangaza kuwa Jumapili, ni siku ya watu wa Roma ya kupumzika. Alitangaza kuwa shughuli mbalimbali za watu zisimame siku hiyo na watu wapate muda wa kupumzika, isipokuwa watu wanaofanya kazi za mashambani kutoka na umuhimu wa shughuli wanayofanya.
Utamaduni huu ndio tunaotumia hadi hivi leo, lakini ni wangapi walifahamu au kutaka tu kujua kwanini siku ya Jumapili ni siku ya mapumziko, tena katika nchi nyingine hulindwa na sheria za nchi kabisa.