Fahamu: Adamu sio wa mtu kwanza kuumbwa

HomeElimu

Fahamu: Adamu sio wa mtu kwanza kuumbwa

Dini zinatupa ukomo wa kufikiria kwa sababu zinaambatana na imani. Hatuwezi kuhoji sana au kwa undani kwa hofu ya ‘kukufuru’, hivyo mara zote tumekuwa tukichukua mafundisho ya dini kama yalivyo na kuishi nayo ndani ya maisha yetu.

Lakini ni kweli Mungu ametuwekea mipaka ya kufikiria na kuwaza kwa undani? Hatudhani, Mungu alituleta Duniani kukiwa tupu zaidi ya miti, mito, bahari, milima na kadhalika alivyoumba kwa matakwa yake, lakini fikira za Mwanadamu alizotunukiwa na Mungu, zimeigeuza Dunia kwa kujenga majengo na vitu vingine vilivyobadili muonekano wa Dunia.

Lazima tutumie akili zetu kung’amua mambo kwa minajili ya kufanya maisha yetu yawe mepesi na mazuri duniani. Umewahi kujiuliza Je, ni kweli Adamu yeye ndio alikuwa mwanadamu wa kwanza? Na vipi kuhusu mifupa inayogunduliwa hivi leo na kupimwa kisayansi kuwa ni mikongwe kuliko Adamu?

Soma upate maarifa, lengo sio kudhihaki dini, bali kufanya tafakuri juu ya kile tunachokiamini. Mwanzo wa kupata mashaka na kukosa majibu juu ya imani zetu, basi ndio mwanzo mzuri wa kusoma zaidi.

Bibilia inatwambia Adamu aliishi miaka 4000 kabla ya Kristo, na kama ni kweli Adamu ndio mwanadamu wa kwanza, basi Bibilia inatofautiana kabisa na Sayansi inasema kwamba, Mwadamu alishakuwepo mapema sana duniani akifanya shughuli zake kabla ya muda wa miaka 4000 kabla ya Yesu kuzaliwa.

Wanasayansi hawaamini hata chembe kwamba eti hakukuwa na watu kabla ya Adamu ambapo Bibilia yenyewe inasema aliishi miaka 4000 iliyopita.

Wataalamu wa takwimu za idadi ya watu wanatwambia kuwa miaka 4000 iliyopita kabla ya Kristo dunia ilikuwa na watu milioni 7. Watafiti wa kihistoria wanaafukua mifupa na miji ya miaka 4000 iliyopita na hata zaidi ya hapo. Mfano Mji wa Catalhayok Uturuki, mji uliojengwa kati ya miaka 5200 – 7400 iliyopita, mji una ekari 37, na ni 5% za mji huo ndio umefukuliwa, una majengo 160 na hizo 5% zimefukuliwa ndani ya miaka 60 ambapo inasemekana idadi ya watu hapo ilikuwa ni kati ya 3000 – 8000.

Hata kwenye Bibilia upo mji wa Jericho Palestina, mji ambao ulikuwepo miaka 10000, maana yake ni mkongwe zaidi kwa miaka 6000 zaidi ya Adamu. Watafiti wa historia wamefukua tayari kama 20 ya mji huo na wamekuta maiti nyingi zikiwa zimezikwa ndani ya nyumba hizo, nazo ni kongwe zaidi ya Adamu.

Bado wanasayansi wamefufua mifupa mingi ya watu ambao kwa asilimia kubwa wanafanana na watu wa leo (homids), na mifupa mingine ina umri mkubwa zaidi ya miaka milioni ishirini.

Kuna hoja kadhaa tukuache nazo ambazo utang’amua:

  1. Kwenye agano la kale, hakuna sehemu yeyote inayoonesha kuwa Adamu alikuwa binadamu wa kwanza
  2. Yesu hakuwahi kumtaja Adamu hata mitume badala yake, isipokuwa Paulo ambaye anamtaja kwa uchache katika Wakorinto 15 Warumi 15 lakini hasemi pia kama alikuwa ndiye Mwanadamu wa kwanza, isipokuwa tu ndio alikuwa mtenda dhambi wa kwanza.
  3. Wanasayansi wamefukua miji mikongwe zaidi ya umri wa Adamu
  4. Hivi sasa ziko njia za kisayansi za kupima umri wa vitu na ushahidi unaonesha dunia ilikuwa na watu nyuma zaidi ya umri wa adamu, kutokana na ushahidi wa mifupa.
error: Content is protected !!