HomeElimu

Wajue nyoka 10 hatari zaidi duniani

Kwa mujibu wa Shirika la Afya la Dunia, kuna nyoka zaidi ya 600 wenye sumu duniani, lakini kati hao ni 200 tu ndio ambao wanaweza kuwa hatari zaidi. Bila kupoteza muda, Click Habari inakuletea Nyoka 10 ambao hao ni hatari zaidi kuliko wote duniani.

1. Inland Tipan
Nyoka huyu sumu yake ni hatari sana, sumu yake ina uwezo kwa kufanya mtu akavuja ndani kwa ndani. Mishipa ya damu na misuli inapasuka, damu inavuja kwa wingi ndani na pumzi kukata ghafla. Chini ya saa moja mtu anaweza kupoteza maisha, na asilimia 80% ya watu walioumwa na nyoka huyu wamefariki.

2. Eastern Brown Snake
Anapatikana sana nchini Australia na New Guinea. Nyoka huyu anasifika kwa kasi analiyonayo na wana urefu wa wastani futi mbili. Huko Australia anahusika na ajali 60% za watu kuumwa nyoka. Akihisi hatari husimama na hukaa umbo la ‘S’ tayari kwa kushambulia. Sumu yake huathiri mfumo mzima wa mzunguko wa damu, hupasua mishipa, shinikizo la damu na shambulio la moyo.

3. Coastal Taipan
Anapatikana sana Australia na New Guinea, madhara ya sumu yake yanafanana na nyoka namba 2. Huyu huwa mrefu na mwembamba, huyu anasifika kwa mashambulizi ya kushtukiza. Huwa ana kawaida ya kuruka na kushambulia akiona hatari. Huyu sumu yake huathiri pia mfumo wa damu na shambulio la moyo.

4. King Cobra
Huyu ni nyoka mrefu zaidi kuliko wote kwa nyoka wenye sumu, urefu wake hufika hadi mita 5.5. Huyu hupatikana sana Asia, hasa India, Indonesia na Thailand. 50% ya watu walioumwa na nyoka huyu wamefariki, sumu yake ni hatari kiasi kwamba akimuuma Tembo mkubwa anaweza kupoteza maisha ndani ya saa chache.

5. Black Mamba
Nyoka huyu anapatikana Afrika ya Mashariki, ana kasi sana na anajulikana kama nyoka mwenye kasi zaidi duniani. Urefu wake hufika hadi mita 4, mwembamba na anaweza kukimbia 19km kwa saa. Ukichanganya kasi aliyonayo na ukali wake kwa adui, humfanya kuwa nyoka hatari zaidi Afrika. Tofauti na nyoka wengine, huyu hujitenga kabisa na binadamu, lakini wakikorofishwa huwa si waoga kukimbia, husimama na kupigana.

6. Barba Amarilla
Hawa makazi yake sana huko Hispania na urefu wao mara nyingi ni mita 1.8, majika ni warefu zaidi na wanene wenye vichwa vipana. Hawa pia wana kasi sana na sumu yao husababisha damu kusimama mwilini.

7. Braded Krait
Huyu hupatikana sana India na Kusini mwa Asia. Urefu wake hufika mita 2, ana rangi ya dhahabu na madoa meusi. Nyoka huyu ni mwenye aibu, na ni nyoka mwenye uwezo wa kuona usiku tu. Si kawaida kuvamia mtu au mnyama, lakini kama akilazimika, sumu yake inaweza kukata pumzi na kupaliwa kusiko kawaida. Uwezo wake wa sumu yake kusababisha kifo 10%.

8. Boomslang
Huyu ni maarufu Kusini mwa bara la Afrika na urefu wake hufika hadi mita 1.6. Huyu umbo lake ni tofauti kidogo, macho yake makubwa na kichwa umbo la yai. Jina lake linatokana na lugha ya Afrikaans likiwa na maana ya ‘Nyoka Mti’ kutokana na mtindo wake wa kushambulia. Huyu akining’inia kwenye mti hutulia bila kutingishika kama tawi la mti kisha kushambulia kwa kasi ya ajabu. Huyu akiuma mtu damu huganda ndani ya muda mchache na kupoteza maisha.

9. Saw Scaled Viper
Huyu huongoza kusababisha vifo vingi kila mwaka huko India. Wanasayansi wanaamini kuwa nyoka huyu husababisha vifo vingi zaidi duniani kuliko nyoka wote ukiwachanganya kwa mwaka. Huyu hupenda kuishi mazingira ya watu, ni mkali na anayeshambulia kwa kushtukiza.

10. Tiger Snake
Huyu ni hatari sana, ila yuko kwenye athari ya kutoweka huko Kusini mwa Australia. Sumu yake inaweza kukusababishia damu kuganda, mishipa ya damu kupasuka, mwili kupooza na shinikizo la damu kwa muda mmoja. Huko Australia anahusika na 17% ya vifo vyote vinavyosabishwa na nyoka.

error: Content is protected !!