Nuno Espirito afungashiwa virago Tottenham

HomeMichezo

Nuno Espirito afungashiwa virago Tottenham

Klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza imemtimua kocha wake mkuu, Mreno Nuno Espirito baada ya mfululizo wa matokeo mabovu katika Ligi Kuu ya England.

Nuno amefungashiwa virago baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Manchester United kufungwa goli 3 kwa 0 katika Uwanja wa Old Trafford siku ya jana. Nuno amepoteza michezo minne kati ya sita ya Ligu Kuu Uingereza.

Tottenham inashika nafasi ya 8 katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa alama 10 nyuma ya vinara wa ligi Chelsea.

Nuno (47) alisaini kandarasi ya miaka miwili Juni mwaka huu kuifundisha Tottenham akichukua nafasi ya Jose Mourinho.

error: Content is protected !!