Mambo 5 muhimu ya kufanya baada ya Kuchepuka

HomeElimu

Mambo 5 muhimu ya kufanya baada ya Kuchepuka

Kuchepuka hakufanyi mahusiano yenu yaishe ila yataisha ikiwa hamtaki tena kuendelea nayo au kutokana na maumivu ambayo aliekosewa anayapata, Kuna sababu mbalimbali zinazowafanya wanandoa au watu waliokuwa kwenye mahusiano wachepuke ikiwemo kutokuridhika na anavyopata kwenye hayo mahusiano. Kuna mambo ambayo unaweza kufanya ili kurekebisha ndoa au mahusiano yaliyovurugika kwasababu ya kuchepuka

  1. Tafakari Jinsi Unavyojisikia
    Jiulize maswali kuhusu nafsi yako na uwe kweli kwa vile unavyojisikia kuhusu mahusiano yako na kosa ulilofanya, unachotakiwa kujiuliza ni kweli unajuta kwa ulichokifanya na uko tayari kuwajibika na kuhakikisha mahusiano yako yanarudi kama mwanzo kama ni ndio basi ni vyema ukajaribu kurudisha mahusiano yako ila kama ni Hapana basi acha kwani utaendelea kumuumiza mwezi wako kwa kuchepuka.
  2. Usirudie kuchepuka
    Moja ya njia rahisi ya kuponya mahusiano yako na kurudisha sehemu ya imani kwa mpenzi wako ni kuacha kuchepuka, Inaweza kutokea mtu uliechepuka nae akavutiwa zaidi na wewe na kutaka kuendelea kuchepuka unatakiwa kutengeneza mazingira yatakayomfanya asiwe karibu na wewe ili kupunguza vishawishi.
  3. Kubali kosa na uwajibike
    Kama una nia ya kuendelea na hayo mahusiano basi unatakiwa ukubali kama kweli ulikosea kuchepuka na una wajibu wa kutengeneza upya mahusiano hayo, Usitoe visingizio kwa mpenzi wako ili aonekane yeye ndo mkosaji wakati wewe ndie ulikosa uaminifu unaweza kufanya vitu kama kuomba msamaha, kumfanyia mpenzi wako vitu anavyovipenda na kutumia muda mwingi kukaa nae kama atahitaji ili arudi kwenye hali yake ya kawaida ila kama atataka umuachie nafasi muache.
  4. Kuwa mwaminifu
    Wanasema ukigongwa na nyoka hata ukishikwa na jani lazima ushtuke ni hivyo hivyo kwa mtu aliesalitiwa anakosa kujiamini muda wote anapata hisia hasi, Uaminifu wako utamfanya apunguze kukufikiria vibaya ukiaga unaenda sehemu basi akipiga simu au akikufata akukute sehemu uliomwambia pia unapoahidi kufanya kitu kitimize na pia uwe muwazi kwake.
  5. Zungumza na mwenza wako
    Ili ndoa yako au mahusiano yadumu na wewe uachane na michepuko zungumza na mpenzi wako kwenye mapungufu yake ikiwa ndio sababu ya wewe kuchepuka, Kuzungumza kutasaidia kujua nini manatakiwa mfanye kama wapenzi ili kuimarisha mahusiano yenu ukimya utavunja ndoa au mahusiano.
error: Content is protected !!