TRC wafunguka kuhusu video ya treni inayosambaa mtandaoni

HomeKitaifa

TRC wafunguka kuhusu video ya treni inayosambaa mtandaoni

Kutokana na video inayosambaa kwa kasi mtandaoni ikionesha treni ya Shirika la Reli Tanzania kutokea Kigoma kuelekea Dodoma ikiwa imechoka kiasi cha kupelekea abiria kusafiri katika mazingira magumu, Shirika la reli Tanzania (TRC) limesema wananchi wapuuzie kwani treni inayoonekana hapo ni ya mwaka 2016.

Mkurugenzi wa TRC, Masanja Kadogosa amelazimika kulitolea ufafanuzi jambo hilo wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kuendelea kuwepo kwa safari za treni kwenda Moshi.

“Puuzeni video ile, kwani haina ukweli wowote. Tumeziboresha treni zetu kwa kiasi kikubwa na mnachokiona pale ni hali ilivyokuwa mwaka 2016, lakini sasa hali ni tofauti kabisa kwani Serikali imeshatoa hela nyingi katika kuboresha usafiri huo,” amesema Kadogosa.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema maneno yanayosemwa kwamba treni hiyo ilikuwa haifanyi kazi sio ya kweli kwani kwa miaka mitatu tangu ifufuliwe haijawahi kusitishwa zaidi ya mwaka juzi palivyotokea mafuriko.

error: Content is protected !!