Jada: Sikutaka kuolewa na Will

HomeBurudani

Jada: Sikutaka kuolewa na Will

Baada ya Will Smith kufungiwa kushiriki Tuzo za Oscars kwa miaka kumi kwa kuonekana kuchukulia ‘serious’ utani wa mchekeshaji Chris Rock kuhusu mke wake Jada Pinkett-Smith, walimwengu wameamua kufukua makaburi kumhusu bibiye.

Kati ya mambo wanayokumbusha watu ni Pinkett-Smith kuzungumza hadharani katika kipindi chake cha Red Table Talk akiwa na mama yake, Adrienne Banfield-Norris (Gammy), mumewe Will na binti yake Willow Smith kuwa hakutaka kuolewa na mumewe huyo wenye watoto wawili pamoja, miaka 23 na 21.

“Nilishinikizwa, unajua, nilikuwa mwigizaji mchanga, bado mdogo, mjamzito na sikujua la kufanya.

“Sikuwahi kutaka kuolewa,” aliongeza Pinkett-Smith.

Oscars: Smith afungiwa miaka 10

Alienda mbali na kumwambia bintiye kuwa mama yake ndiye aliyemlazimisha aolewe na Will baada ya kupata mimba.

“Harusi ilikuwa mbaya,” mama mkwe alisema. “Mbaya haswa. Jada aliumwa, hakupendezwa sana… hakujishirikisha na chochote.” Akicheka, Pinkett-Smith alikubali, akisema, “Na nilikasirika sana kwamba nililazimika kufanya harusi. Nilikasirika sana nikalia safari nzima kwenda jukwaani.”

Will Smith akiwa mnyonge na kuongea kwa busara alisema “Hakuna siku katika maisha yangu ambayo nilitaka chochote zaidi ya kuoa na kuwa na familia. Kuanzia umri wa miaka 5, nilikuwa nikiwaza jinsi familia yangu ingekuwa.”

Will Smith aomba msamaha

Pigo lingine kwa Will ni baada ya aliyekuwa hawara wa mkewe, mwimbaji August Alsina (29) kusema kuwa anatarajia kuzindua kitabu chake ambacho ndani yake amezungumzia kwa kina mahusiano yake ya kimapenzi na Jada.

error: Content is protected !!