PISHI: Jinsi ya kupika vipopoo vya Iftar

HomeElimu

PISHI: Jinsi ya kupika vipopoo vya Iftar

Katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ambapo Waislam hufunga kwa sala, sadaka na kujinyima pia, ni kipindi ambacho huendana na aina fulani ya chakula vingi vikiwa ni vyakula vyenye sukari zaidi ile jioni wakati wa iftar.

Moja kati ya vyakula pendwa kipindi hiki cha Ramadhani ni vipopoo ambavyo huliwa zaidi Zanzibar na hii ndiyo namna ya kuviandaa vipopoo vyako;

Mahitaji

  • Unga wa ngano vikombe 2
  • Unga wa sembe vjk 2 (si lazima)
  • Tui la Nazi vikombe 3
  • Maji kikombe 1.5
  • Sukari ya kutosha ladha yako
  • Chumvi kidogo kwaajili ya ladha
  • Iliki kjk 1
  • Mdalasini kidogo usiosagwa.

Jinsi ya kupika

  1. Tenga sufuria yenye maji kikombe kimoja na nusu jikoni
  2. Changanya unga wa ngano vikombe viwili na usonge mchanganyiko wako hadi uive kama ugali bila vitoto.
  3. Epua mchanganyiko wako ukande kidogo ili usigande
  4. Ugawanye katika madonge madogo madogo na kisha anza kuvikata vipande vidogo vidogo kama gololi kwa kushika na unga wa ngano pembeni ili usinatenate.
  5. Chukua tui lako la nazi na utenge jikoni kwenye sufuria, tia unga wa ugali vijiko viwili, iliki, chumvi, sukari yako ya kutosha kwa ladha, na mdalasini.
  6. Koroga tui lako mpaka liive, kisha tia vipopoo vyako na uviache vichemke hadi vianze kugandaganda na kuwa vizito.
  7. Epua sufuria yako jikoni kisha ondoa magome ya mdalasini ulioweka kwaajili ya ladha na harufu tayari kwa kupakua na kula.

Unaweza kula vipopoo vikiwa vya moto au vya baridi.

Jinsi ya kutengeneza jamu ya machungwa

error: Content is protected !!