Rais Samia aibuka kinara

HomeKimataifa

Rais Samia aibuka kinara

Rais Samia Suluhu Hassan ametangazwa mshindi wa tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 baada ya viongozi na watu mashuhuri kutambua mchango wake katika uboreshaji wa miundombinu.

Kamati ya uandaaji wa tuzo hiyo imesema wameona mchango mkubwa wa Rais Samia katika kuboresha miundombinu na usafirishaji na ndio maana ikaamua apewe ushindi huo mwaka huu.

Kamati ilibaini dola milioni 290 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kusaidia ufufuaji wa usafiri wa barabara, reli na anga nchini Tanzania, ilizingatia mkataba wa dola milioni 172.2 uliosainiwa na Kampuni ya China Corporation Limited kuipatia nchi mabehewa ya kisasa ya mizigo 1,430 ili kutekeleza mpango kabambe wa shirika la reli la Tanzania. 

Hatimaye kamati ilibaini kuanza rasmi kwa ujenzi wa mradi wa kihistoria wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje kuzunguka mji wa Dodoma, mradi huu ulizinduliwa na Rais Hassan tarehe 11 Februari, mbele ya Rais wa Kundi la Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dk. Akinwumi A. Adesina.

Tuzo hiyo ilianzishwa kwa heshima ya Babacar Ndiaye, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kutoka 1985 hadi 1995 na mwaka huu atakabidhiwa Rais Samia katika mkutano wa mwisho wa Wajenzi wa Barabara Afrika ambapo umepangwa kufanyika na Benki ya Maendeleo ya Afrika

error: Content is protected !!