Jeshi la Polisi laanza kuichunguza Kalynda

HomeKitaifa

Jeshi la Polisi laanza kuichunguza Kalynda

Jeshi la Polisi limeanza kuchunguza tuhuma za utapeli kwa njia ya mtandao dhidi ya kampuni ya Kalynda e-Commerce.

Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime amesema, Jeshi limepokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu kutapeliwa fedha zao na kampuni hiyo na kwamba Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai inashirikiana na taasisi nyingine za kiuchunguzi na za kifedha.

“Hatua zinaendelea kuchukuliwa, Jeshi la Polisi lingependa kutoa tahadhari tena kwa mara nyingine kwa watanzania … kila mmoja atambue maendeleo ya sayansi na teknolojia, wengine wanajifanya kuuza bidhaa za aina mbalimbali au magari,” amesema SACP Misime.

error: Content is protected !!