Rais amfukuza kazi waziri mkuu akihofia kupinduliwa

HomeKimataifa

Rais amfukuza kazi waziri mkuu akihofia kupinduliwa

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye amemfuta kazi waziri mkuu na msaidizi wake mkuu katika msako mkubwa jana baada ya kuonya kuhusu njama za mapinduzi dhidi yake.

Alimfukuza kazi waziri mkuu wake Alain Guillaume Bunyoni na mkuu wake wa baraza la mawaziri, Jenerali Gabriel Nizigama kwenye siku ya taharuki katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki iliyogubikwa na machafuko.

Kuondoka kwa Bunyoni kulikuja baada ya Ndayishimiye, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka miwili, wiki iliyopita kuonya kuhusu njama za kufanyika mapinduzi dhidi ya utawala wake.

 

error: Content is protected !!