Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus. Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.
Kama tayari mtu ana tatizo la vidonda vya tumbo inashauriwa atumie vyakula vifuatavyo kupunguza maumivu au hata kuzuia hali ya vidonda hivyo kuwa mbaya zaidi.
1. Asali
Asali ina kemikali au madini fulani iitwayo ‘flavonoids’ ambayo inaaminika kwamba ina umuhimu kubwa sana kwenye tiba ya vidonda vya tumbo. Kemikali hii husaidia kupunguza uzalishaji wa kemikali ambayo inakwenda kuunguza mashambulizi kwenye kuta za tumbo.
2. Vitungu Saumu
Helicobacter pylori(H. pylori) ni bakteria ambao wanaweza kuingia ndani ya mwili wa mwanadamu na kusababisha vidonda na michubuko. Bakteria hawa wanaweza kuishi kwenye kuta za utumbo wa mwanadamu na wanaweza pia kupelekea mtu kuugua saratani ya utumbo. Kitunguu saumu ni dawa nzuri sana ya kuzuia bakteria hawa kuzaliana ndani ya tumbo. Sio lazima viitafunwe vizima, bali unaweza kutumia kwenye chakula na hata kutia kwenye chai.
3. Broccolli
Mboga nyingi za majani kama Broccolli, spinachi, chinese na nyinginezo zina utajiri mkubwa wa Vitamini A. Vitamini A mwilini huongeza uzalishaji wa musuc/ utete ambao hulinda kuta za utumbo dhidi ya mashambulizi.
4. Kranberi (Cranberry)
Kranberi ina madini yanayoitwa polyphenols ambayo ni mazuri kwa kupunguza uzalianaji wa bakteria wanaoshambulia kuta za utumbo tumboni. Pia juice ya Kranberi kama itatumiwa mara kwa mara hupunguza maumivu ya vidonda vya tumbo.
5. Yoghurt
Yoghurt wataalamu huuita ‘probiotics’, hawa ni bacteria wazuri wenye faida kubwa sana mwilini hasa kwenye mmeng’enyo wa chakula. Yoghurt zinapunguza uzalianaji wa bakteria wanaoshambulia kuta za tumbo, na pia kuchagiza uzalishaji wa music/utete unaosaida kupunguza mashambulizi dhidi ya ukuta.