Bangi imelimwa miaka mingi sana barani Afrika, licha ya kwamba nchi nyingi zimekuwa na sheria za kuzuia utumiaji wa zao hilo, sheria ambazo zilirithiwa kutoka kwa wakoloni.
Zao la bangi barani Afrika limeanza kushika taswira mpya baada ya zao hilo kuanza kujitajika kwa wingi duniani kwa ajili ya matibabu.
Kuna wimbi kubwa la mataifa makubwa duniani kote kuruhusu bangi aidha kwa matumizi ya matibabu au kama starehe tu, soko la bangi linakuwa kwa kasi.
Soko la Dunia linatarajiwa kufikia dola bilioni 43 ifikapo mwaka 2024, kwa Ulaya peke, 2027 mahitaji ya bangi yanatarajiwa kufikia thamani ya dola bilioni 37 ambapo mwaka 2019 ilikuwa ni dola bilioni 3.5.
Soko la Bangi barani Afrika linaweza kufikia Sh. Trilioni 15 kwa mwaka hadi kufikia 2023, kama ikiwa mataifa makubwa ya masoko makubwa ya duniani yapatisha sheria ya kuhalilisha bangi.
Utafiti huu umefanywa na ‘The African Cannabis Report’. Inakadiriwa kuwa Afrika inavuna Bangi tani 38,000 kwa mwaka licha ya kuwa zao hilo ni haramu.
Zifuatazo ni nchi zilizoruhusu kilimo cha Bangi barani Afrika
1. Mwaka 2017, Taifa la Lethoto lilikuwa la kwanza barani Afrika kutoa leseni ya ulimaji wa bangi kwa ajili ya biashara na tafiti za kisayansi.
2. Zimbabwe
3. Afrika Kusini
4. eSwatini
5. Zambia
6. Uganda
7. Zambia
8. Rwanda
9. Ghana