TAKUKURU yashikwa pabaya wizi wa madini Mererani

HomeKitaifa

TAKUKURU yashikwa pabaya wizi wa madini Mererani

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Mohammed Mchengerwa, ametoa wiki mbili kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), kufuatilia wizi wa madini katika mgodi wa serikali wa Mererani ulioko mkoa wa Arusha.

Kadhalika, ameagiza taasisi hiyo pia kuchunguza ubadhirifu wa fedha za umma kati katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Waziri Mchengerwa amesema kuwa kumekuwa na maneno kila kona kuhusu wizi wa madini katika mkoa wa Manyara na Arusha ambayo inasababishia Taifa hasara kubwa.

“Nawapatia wiki mbili kuhakikisha mnafanya uchunguzi wa kina ili kubaini wezi wa madini hayo, tunahitaji kuona Taifa linakuwa kiuchumi nasi kusikia wezi wanaorudisha maendeleo nyuma,” alisema mchingerwa.

error: Content is protected !!