Kanisa moja la kigeni linalojulikana kama Akorino lililopo kata ya Nanjara, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro. limewapiga marufuku waumini wake wajawazito kuhudhuria kliniki kupata huduma za uchunguzi, kujifungulia hospitalini, kutumia dawa tiba pamoja kuzuia watoto kwenda shule.
Pamoja na hayo wanawake wanaofiwa na wanaume zao hawaruhusiwi kuolewa tena, isipokua hutafutiwa mwanaume ambaye ni muumini katika kanisa hilo. Kutokana na hali hiyo wakazi wa Rombo wameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kufanya uchunguzi wa kina juu ya dhehebu hilo na kuchukua hatua stahiki ili kulinda ustawi wa nwananchi wa maeneo hayo.
Mwanaharakati Beatrice Jackob mkazi wa Njara alisema “Hilo kanisa la wakorino limetokea nchi jirani (Kenya) na hivi sasa limeanzishwa na lipo eneo la kibaoni, kata ya Nanjara. Linazuia wajawazito kwenda kliniki ama kwenda hospitali au watoto kwenda shule”. Alisema Beatrice
“Au ukiumwa unafanyiwa maombi na sio kwenda hospitali aua kumeza dawa yeyote inatushangaza kwa sababu kuna mjamzito alikua na mumewe mgonjwa hakwenda hospitali wakasema wanamfanyia maombi mpaka akafariki. Hilo kanisa bado lipo na linaendelea kufanya maombi nyumbani kwa mtu mmoja pale Nanjara” aliongezea Beatrice
Aidha pia mzee wa mila wa eneo hilo Daudi Silayo alisema “Mtu akifariki dunia kulingana na imani ya wanaosali katika kanisa hilo, tumoena juzi juzi, ukifa wanazika siku hiyo hiyo kama umefariki mapema na juuu ya kaburi lako wanaotesha migomba hawataki kuwe na alama ya kaburi. Ukipita hapo huwezi kujua kama kuna mtu amezikwa”