Madalali sasa ni rasmi, kuanza usajili Januari 2022

HomeKitaifa

Madalali sasa ni rasmi, kuanza usajili Januari 2022

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi ametoa mwongozo wa kusimamia shughuli za udalali nchini ili kuwatambua, kutambua shughuli zao, kufahamu mahali wanapofanyia kazi, utaratibu wa kuratibu, kudhibiti shuguli zao za udalali na kulinda na kulinda maslahi ya wateja, wamiliki, madalali na serikali.

Lukuvi alisema kwamba mwongozo huo unamtaka kila dalali anayepangisha, kuuza kiwanja ama au kupangisha nyumba kusajiliwa na usajili huo utafanyika kuanzia Januari hadi Machi, 2022 huku akitaja vigezo na sifa ambazo madallai watatambulika kupitia mwongozo huo ni kuwa raia wa Tanzania mwenye akili timamu na umri usiopungua miaka 18, anuani au namba ya simu au utambulisho kwa mfumo wa kielektroniki(barua pepe), mahali pa kufanyia kazi panapofahamika.

“Kupitia mwongozo huo utambuzi wa madalali utafanywa na idara mpya ya Mipango Miji na Mazingira katika miji na katika halmashauri za wilaya,” alisema Lukuvi.

Aidha, aliongezea kwa kusema kuwa baada ya utaratibu kukamilika, halmashauri husika itampa mwombaji utambulisho wa kufanya shughuli za udalali wa nyumba/majengo, viwanja na mashamba na kusisitiza mtu au kampuni yoyote itatakiwa kufuata taratibu ikiwemo kujaza fomu ya maombi ya usajili, kuwasilisha barua ya utambulisho kutoka Serikali za Mitaa na kulipa ada ya utambulisho Sh 20,000 kwa kila mwaka.

error: Content is protected !!