Watu maarufu walionunua magari 2021

HomeBurudani

Watu maarufu walionunua magari 2021

Mwaka 2021 umekuwa na changamoto kwa wengi ikiwa ni pamoja na janga la Covid- 19, biashara nyingi zilikwama na nyingine kuwa vilema hali iliyofanya maisha kuwa magumu zaidi kwa wengi.

Hata hivyo, licha ya hali ngumu ya kiuchumi watu kadhaa maarufu wamebahatika kusalia na kuvuna matunda ya kazi zao ngumu, ili kujithamini kwa bidii na kujitolea kwao, wachache waliamua kujizawadia zawadi mbalimbali ikiwemo magari.

Wafuatao ni baadhi ya watu maarufu walionunua magari mwaka 2021

1. Diamond Platnumz
Julai 2021, Mkurugenzi Mtendaji wa Wasafi amejizawadia  Rolls-Royce Cullinan ya 2021 ikiwa ni miongoni mwa magari ya kifahari zaidi duniani. Kulingana na mahitaji ya mtu binafsi, makadirio ya bei ya gari ni kati ya Sh 50 milioni hadi Sh90 milioni.

Mwezi mmoja kabla ya hapo, Diamond alijinunulia toleo jipya la Cadillac Escalade Black gari ambalo ndani ni kama ndege binafsi.Magari hayo mawili yanaunda kundi la magari ya kifahari ambayo mwimbaji huyo anamiliki.

2. Davido
Davido amejizawadia gari mpya aina ya Lamborghini Aventador kama zawadi ya krismasi lenye thamani ya Sh 62 milioni. Davido anafahamika kuwa na magari mengi ya kifahari lakini baada ya kununua hili amesema kuwa anapunguza kazi ya ununuzi wa magari.

“Ninaahidi hilo lilikuwa la mwisho. Hakuna magari tena kwa muda,” alisema Davido.

3. Jux
Msanii huyu wa Bongo fleva na yeye hakuwa nyuma kwani ameweza kujinunulia gari aina ya Mercedes Benz mwezi Juni lakini pia mwaka huu umekuwa na baraka kwake kwani ameweza kufungua rasmi duka lake la nguo maeneo ya Sinza.

4. Nandy
Msanii wa kike wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga au Nandy ameshindika na hakamatiki kutokana na spidi ya mafanikio anayoyapata kila kukicha ikiwemo kujizawadia ndinga kali na la kifahari aina ya Range Rover Evoque.

Hili sio gari la kifahari la kwanza kumilikiwa na msanii huyu, Baadhi ya magari mengine ya Nandy ya kifahari ni pamoja na Land Rover Discovery TDV6 HSE, BMW X1, Mercedes Benz E-Class E320 CDI, Toyota Alphard, Toyota Harrier na Toyota Noah ambayo anayatumia kwa shughuli zake mbalimbali.

5. Maua Sama
Maua anatamba sasa na wimbo wake wa Zai ambao unafanya vizuri kwenye chati tofauti hivi karibuni nayeye amejinunulia zawadi gari aina ya Vanguard ikiwa ni kati ya ndoto zake alizokuwa anatamani kutimiza kumiliki gari lake mwenyewe.

6. Marioo
Marioo a.k.a Toto Bad yeye pia amevuta ndinga kali la kifahari aina ya BMW X1, kwa sasa nyota huyu anayetamba kwa ngoma yake ya Beer Tamu inayofanya vizuri nchini na kufungisha mwaka kama wimbo unaopendwa na kuchezwa sana kwenye sherehe au mikusanyiko mbalimbali.

error: Content is protected !!