Panya Road walivyokamatwa na Polisi

HomeKitaifa

Panya Road walivyokamatwa na Polisi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema wahalifu sita wa unyang’anyi wa kutumia silaha wamefariki dunia baada ya kujeruhiwa wakijaribu kuwakabili polisi walioyaka kuwakamata.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro alisema jana watu hao walijeruhiwa juzi saa 4:15 usiku katika eneo la Makongo area 4.

Kamanda Muliro alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kulikuwa n akundi la watu tisa waliokuwa katika gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 260 BEP wakitoka Mabibo wakiwa na mapanga na zana nyingine za kuvunjia na kufanya uhalifu, wakienda Goba Kinzudi, Wilaya ya Ubungo kuvamia nyumba kadhaa na kupora mali usiku huo.

Alisema polisi walipofika Makongo, walikutana na gari hilo na walipolizuia, watuhumiwa hao walishuka na kuanza kuwatishia kwa mapanga askari polisi wakipinga kukamatwa.

“Na katika mazingira hayo, askari walijihami kwa kufyatua risasi kadhaa hewani lakini wahalifu hao waliendelea kukaidi na kutaka kuwajeruhi polisi, ndipo walishambuliwa, kujeruhiwa na baadaye walipelekwa haraka hospitali lakini walipoteza maisha,” alisema Kamanda Muliro.

Alisema watuhumiwa watatu walikimbia na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawasaka.

Kamanda Muliro alisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa watu wawili kati ya hao, ni viongozi wa kundi hilo na wametambuliwa kwa majina ya Salum Juma Mkwama maarufu babu salum anayekadiriwa kuwa na umri kati ua miaka 27 na 30 ambaye ni mkazi wa Mbagala.

Pia alisema upelelezi wa awali ulibaini kuwa watuhumiwa hao waliotambuliwa, walidaiwa kushiriki tukio la mauaji la Septemba 14 mwaka huu usiku Kawe Malingo na matukio mengine ya kuvunja  nyumba usiku, kujeruhi kwa mapanga na kupora mali yaliyotokea siku za karibuni.

Kamanda Muliro alisema Jeshi la Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam litaendela kutekeleza maelekezo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Camilius Wambura ya kuhakikisha mifumo ya usalama na kisheria inazingatiwa usalama urejeshwe haraka Dar es Salaam.

 

error: Content is protected !!