Afariki kwenye ajali akimkimbiza mumewe na mchepuko

HomeBurudani

Afariki kwenye ajali akimkimbiza mumewe na mchepuko

Mwanamke mmoja nchini Nigeria amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari wakati akimfukuzia mumewe aliyekuwa na mwanamke mwingine kwenye gari.

Kwa mujibu wa shuhuda, mwanamke huyo baada ya kumuona mumewe akiwa na mwanamke mwingine wakitoka saluni ya Kike na kuingia kwenye gari, aliondoa gari yake kwa kasi kwa lengo la kuwahi mbele ili kuwaziba njia.

Baada ya ajali, mumewe alisimamisha gari na kumshusha yule mwanamke aliyekuwa naye na kisha kwenda kumsaidia mkewe ambapo alikimbizwa haraka hospitali lakini baadaye taarifa zilitoka kuwa amefariki dunia.

error: Content is protected !!