Rais Samia chanzo cha ongezeko la mapato

HomeKitaifa

Rais Samia chanzo cha ongezeko la mapato

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Innocent Bashungwa amesema kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji wa mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuatia kufunguka kwa nchi na uwepo wa mazingira wezeshi ya kukuza uchumi nchini.

Ametoa kauli hiyo leo agosti 6, 2022 kwenye ziara ya Rais Samia ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ampao amempongeza Mheshiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua nchi.

Amesema kupitia takwimu za ukusanyaji wa mapato katika mwaka 2021/2022 Mkoa wa mbeya umekusanya kwa asilimia 105.

Amemuhakikishia Rais Samia kushirikiana na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watajipanga vyema kuhakikisha takwimu ya ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 103 itakuwa ni kiwango cha kujipima hadi kufikia asilimia 150.

error: Content is protected !!