Watumishi Tanga wamshukuru Rais Samia kwa nyongeza ya 23.3%

HomeKitaifa

Watumishi Tanga wamshukuru Rais Samia kwa nyongeza ya 23.3%

Watumishi wa Serikali Mkoani Tanga wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mishahara ambao umekwenda sambamba na upandishaji wa madaraja jambo ambalo litawawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari Jijini Tanga, watumishi hao wamesema jambo ambalo (Rais Samia) amelifanya kwao ni kubwa mno hivyo wanamshukuru na wataendelea kumuunga mkono.

Akizungumza mmoja wa watumishi hao katika Jiji la Tanga Mwanaisha Shaka amesema wanamshukuru pia kuwapandisha madaraja kwani wamekaa miaka mingi zaidi ya sita hadi saba bila kupandishwa madaraja lakini kwa sasa jambo hilo limefanyika.

“Tumekaa zaidi ya miaka 7 hatujawahi kupandishwa madaraja lakini sasa Rais Samia Suluhu amepandisha madaraja kwa watumishi wote sie tupo nyuma yake tutafanya kazi kwa bidii,” amesema.

error: Content is protected !!