Rais Samia aelezea kwanini serikali inashirikiana na machifu

HomeUncategorized

Rais Samia aelezea kwanini serikali inashirikiana na machifu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan amesema serikali imeamua kushirikiana na machifu na viongozi wa kimila ili kuwa na jukwaa la pamoja baina ya Serikali, machifu na wazee wa kimila. Ushirikiano huo unalenga kuhifadhi mila na desturi za Kitanzania pamoja na uhifadhi wa maeneo mbalimbali yaliyotunzwa kama njia ya kuhifadhi mazingira hayo yamesemwa leo katika uzinduzi wa tamasha la Utamaduni Moshi mkoani Kilimanjaro.

Uzinduzi wa tamasha hilo ni utekelezaji wa kauli ya Rais Samia alipokua Mwanza ambapo alisimikwa kuwa Chifu Mkuu wa machifu na kupewa jina la Hangaya, Rais Samia alitaka matamasha ya utamaduni yafanyike katika mikoa ili kutunza utamaduni wa kitanzania kwani utamaduni ni Ajira, kivutio cha utalii na Uchumi.

Pamoja na hayo Rais Samia amezielezea juhudi zinazofanywa na serikali kwa upande wa machifu ikiwemo kuanzishwa kwa kanzi data sahihi inayohusu machifu nchini ambapo hadi Januari 20 machifu 92 walikua wamesajiliwa. Maafisa utamaduni mikoa wameagizwa kuwatambua machifu na kuwasilisha taarifa zao wizarani, Idara ya maendeleo na Utamaduni kuanzisha programu ya kuhifadhi taarifa za jinsi makabila na uongozi wao ulivyoshiriki katika kupambania uhuru na kubaini maeneo ya kichifu na kimila ili yawe sehemu ya vivutio vya utalii pamoja na kuhifadhi dhana mbalimbali zilizokua zinatumika zamani.

error: Content is protected !!