Afariki nyumba ya wageni baada ya kuzidisha vidonge vya kuongeza nguvu za kiume

HomeKimataifa

Afariki nyumba ya wageni baada ya kuzidisha vidonge vya kuongeza nguvu za kiume

Polisi nchini Kenya Kaunti ya Homa Bay wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mwanaume mwenye umri wa miaka 55 aliyekutwa amefariki kwenye nyumba ya kulala wageni mjini Ndhiwa Ijumaa usiku kwa kile kinachodaiwa kuzidisha dozi ya kuongeza nguvu za kiume.

Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Ndhiwa, Paul Rioba zimesema kwamba marehemu alikodi chumba kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni kabla kujumuika na mwenza wake wa kike na kusema mwanamke huyo alienda kutoa taarifa kwa uongozi wa baa baada ya marehemu kuzimia wakati wakishiriki tendo la ndoa.

Mwanamke huyo alikiri kushiriki tendo la ndoa na marehemu lakini dakika chache baadae alianza kuzimia na kufariki dunia, huku Polisi wakishuku kuwa huenda mwanaume huyo alitumia vidonge vya Viagra vinavyoongoza nguvu za kiume na kupelekea kifo chake.

Aidha ,Kamanda Rioba alieleza kwamba wanamshikilia mwanamke huyo anayesemekan akuwa na umri wa miaka 25 katika kituo cha Polisi Ndhiwa kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hilo huku mwili wa marehemu ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Manyatta Kobodo.

 

 

error: Content is protected !!