Nuh Mziwanda afuta tattoo ya Shilole

HomeBurudani

Nuh Mziwanda afuta tattoo ya Shilole

Aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki na mjasiriamali Zena Yusuf Mohammed maarufu kama Shilole, msanii Nuh Mziwanda hatimaye amefuta tattoo aliyokuwa ameichora mkononi yenye jina la ‘Shishi Baby’ baada ya miaka mitano tangu wawili hao walipoachana.

Nuh amethibitisha hili baada yakuweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuonyesha tattoo hiyo yenye jina la Shilole na kuandika ujumbe kwamba sasa anaifuta baada ya miaka mitano huku  akukiri kwamba upendo wake kwa Shilole umechelewa kufa.

“Kwa Mara ya kwanza Leo Nafuta Tatoo ya X wangu (2022) Nimekaa nayo Sana almost 5 years (F……………..ck Love) ila upendo Wangu Umechelewa Sana Kufa  ‘Shout out kwa Wote Niliowatengenezea Mazingira Am done Kiroho safi “ ameandika Nuh.

Enzi za mahusiano yao wawili hawa walikua wanakimbiza mitandaoni kwa visa mbalimbali huku wakiripotiwa kuachana na kurudiana zaidi ya mara moja kabla yakuvunja mapenzi yao rasmi.

error: Content is protected !!