Rais George Weah wa Liberia amesababisha taharuki nchini humo baada ya kuzindua kitabu chake huku wanawake nchini Liberia wakijiandaa kuandamana kwa kile kinachodaiwa kuwa ni udhalilishaji, katika moja ya kurasa za kitabu cha Rais Weah imeelezwa sababu ya yeye kumchagua mkewe huyo dhidi ya wanawake wengine kuwa ni uwezo wake chumbani.
Sehemu ya kitabu hiko ambayo inamuelezea (first lady) Clar Marie Weah ilipigwa picha na kusambazwa mtandaoni na mwandishi wa habari wa Liberia Henry Costa aishie Marekani, mpaka sasa Rais huyo wala mkewe hawajazungumza lolote kuhusiana na tukio hilo.
Kitabu hicho mbacho kinamhusisha mwandishi Isaac Vah Tukpah ambaye inasemekana alikuwa na mpango wa kukimbia nchi hiyo baada ya tukio hilo, huku ikidaiwa kuwa Rais Weah alimzuia ili asitoke nje ya nchi lakini baadaye Weah alikanusha na kusema kuwa mwandishi huyo yuko huru anaweza kwenda nchi yoyote atakayotaka na wala hatashitakiwa.
Sintofahamu imebaki nchini humo ikiwa ni kweli Rais Weah aliongea hivyo na alitaka kitabu hicho kiandikwe hivyo au mwandishi alifanya makosa kuandika hivyo.